Taarifa iliyotolewa jana Jumatatu na Igor Konashenkov, Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Russia imeeleza kuwa, makombora manne aina ya AGM-88 High-speed Anti-Radiation Missiles (HARM) ya Marekani yametunguliwa katika anga ya eneo la Belgorod, yapata kilomita 40 kaskazini mwa mpaka wa Russia na Ukraine ndani ya saa 24 zilizopita.
Duru za habari zinaarifu kuwa, serikali ya Washington ilituma nchini Ukraine makombora ya aina hiyo katikati ya mwezi Agosti mwaka huu 2022.
Makombora hayo yaliyozalishwa na Marekani yameripotiwa kuvurumishwa kutoka kwenye ndege za kivita za Ukraine za MiG-29 na Su-27.
342/